Al-Shabab yadai kuwajibika na shambulio la Garissa Kenya
Al-Shabab yadai kuwajibika na shambulio la Garissa Kenya
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa wanajificha ndani ya gari baada ya kukimbia kutoka shambulizi la chuo chao Garissa, Kenya, April 2, 2015.
Kundi la wanamgambo wa Kisomali la Al-Shabab limedai kuwajibika na shambulio katika chuo kikuu cha Garissa kilichopo kaskazini- mashariki ya Kenya, na kusababisha vifo vya watu 147.
Kufuatana na mwandishi wa habari wa Sauti ya Amerika-VOA mjini Garissa, watu 65 wamejeruhiwa na idadi isiyojulikana ya wanafunzi wanashikiliwa mateka na karibu wanafunzi wengine 400 hawajulikani mahala walipo.
Msemaji wa kundi hilo lenya uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda, Sheikh Ali Mohamed Rage, aliliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kwamba wanamgambo wao walishambulia chuo kikuu hicho Alhamisi alfajiri na kuwachukua mateka wanafunzi wote wakristo na kuwaachilia huru waislamu.
Milio ya bunduki ya hapa na pale imekuwa ikisikika saa sita baada ya shambulio hilo, wakati wizara ya mambo ya ndani ya Kenya ikiripoti kwamba washambulizi wamezingirwa katika eneo moja.
Rais Uhuru Kenyatta alilihutubia taifa kueleza kitendo hicho cha Garissa akitoa rambi rambi zake kwa familia za walioathiriwa na kuwahakikishia wananchi kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika na shambulio hilo.
Al-Shabab washambulia chuo kikuu cha Garissa Kenya
1/12Kifaru cha jeshi la Kenya kikiwasili karibu na chuo kikuu cha Garissa,Garissa, Kenya, April 2, 2015.
Onyesha zaidiShow less
2/12Polisi wa Kenya wakikaribia majengo ya chuo cha Garissa kwa uangalifu mkubwa
Onyesha zaidiShow less
3/12Wananchi wa Garissa wakisubiri kuchangia damu katika hospitali ya Garissa ambako wengi waliojeruhiwa wamelazwa
Onyesha zaidiShow less
4/12Kifaru cha jeshi la Kenya katika barabara kuelekea chuo cha Garissa
Onyesha zaidiShow less
5/12Kifaru cha jeshi la Kenya kikiwasili karibu na chuo kikuu cha Garissa,Garissa, Kenya, April 2, 2015.
Onyesha zaidiShow less
6/12Wanafunzi wakikusanyika nje ya chuo kikuu cha Garissa kufuatia shambulio la watu wenye silaha., April 2, 2015.
Onyesha zaidiShow less
7/12Wanafunzi wakitafuta usalama katika chuo kikuu cha Garissa
Onyesha zaidiShow less
8/12Wanafunzi wakitafuta usalama katika chuo kikuu cha Garissa
Onyesha zaidiShow less
9/12Wanafunzi bila ya sharti wakitoka kwenye bweni la chuo kikuu cha Garissa
Onyesha zaidiShow less
10/12Kenya University Attack
Onyesha zaidiShow less
11/12Students of Garissa University College take shelter in a vehicle after fleeing from an attack by gunmen in Garissa, April 2, 2015.
Onyesha zaidiShow less
12/12Maafisa wa polisi wa Kenya wachukua hifadhi nje ya chuo kikuu cha Garissa, April 2, 2015.