Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 09:00

Kenya yatangaza donge la dolla laki 2 dhidi ya Mohammed Kuno


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akihutubia taifa kwenye picha ya maktaba.

Serikali ya Kenya inatoa zawadi ya dola 220,000 kwa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa mwanachama wa kundi al-Shabab aliyeshukiwa kuhusika mashambulizi katika mashambulizi ya Garissa Alhamisi ambapo watu 147 waliuawa.

Mtu huyo, Mohammed Mahamoud Kuno, ambae tayari yupo kwenye orodha ya watu wanaotafutwa na serikali ya nchi hiyo anashukiwa kuwa mkuu wa operesheni za nje wa kundi la al-Shabab dhidi ya Kenya. Pia anajulikana kwa jina la Gamadhere au Dulyadayna.

Kuno anatafutwa ili aweze kuhojiwa kuhusu shambulizi kwenye chuo kikuu chaGarissa mahala ambako washambuliaji walishambulia majengo ya chuo alfajiri ya Alhamis na kufyatua risasi.

Viongozi wa kigeni wamelaani shambulizo hilo na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ametowa wito wa kuwepo na ushirikiano mkubwa zaidi na kenya, alipotoa rambi rambi zake kwa wakenya.

Viongozi wa kigeni wamelaani shambulizo hilo na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ametowa wito wa kuwepo na ushirikiano mkubwa Zaidi na kenya, alipotoa rambi rambi zake kwa wakenya.

XS
SM
MD
LG