Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 16:36

'Al-shabaab' walipua mnara wa mawasiliano Kenya


Kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab

Watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa kikundi cha al-Shabaab wameteketeza mnara wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom nchini Kenya katika kaunti ya Wajir, na kuathiri mawasiliano.

vyanzo vya habari nchini Kenya vimesema kuwa tukio hilo limetokea saa saba usiku wa kuamkia Jumapili.

Mnara huo inasemekana uliwahi kuharibiwa miaka ya nyuma na kikundi hicho.

Katika mahojiano na gazeti la The Nation, Polisi kamanda wa Kaunti ya Wajir Stephen Ng'etich amesema kuwa mlipuko mkubwa ulisikika wakati idadi isiyojulikana ya washambuliaji walipolipua eneo hilo.

Amesema kuwa mlipuko huo uliwafanya maafisa wanaolinda karibu na kituo hicho kutafuta pahala pakuokoa maisha yao wakati hawakujua nini kinatokea.

Muda mfupi baada ya maafisa hao kurejea katika eneo hilo na kuanza kupambana nao kwa risasi.

"Maafisa wetu waliendelea kupambana nao kwa kutupiana risasi waasi hao kabla ya kukimbia," amesema kamanda huyo.

Lakini amesema kuwa hakuna afisa yoyote aliyejeruhiwa katika shambulizi hilo.

"Kwanza kabisa tulikuwa na wasiwasi juu ya kutoweka kwa maafisa wetu kwani tulikuwa tumepoteza mawasiliano nao kabla ya kupeleka timu ya kutoa msaada kutoka vituo vyetu vya Tarbaj na Kutulo na kutufahamisha maafisa wetu wote wako salama.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG