Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:18

Afrika : Ripoti ya WB inaonyesha ukuaji wa uchumi uko chini 2019


Makao Makuu ya Benki ya Dunia
Makao Makuu ya Benki ya Dunia

Ripoti ya Benki ya Dunia (WB) inasema kwamba ukuaji wa uchumi katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, umeendelea kuwa mdogo mwaka 2019, kutokana na misukusuko ya uchumi wa dunia na mabadiliko machache ya kiuchumi katika nchi hizo.

Kulingana na toleo la 20 la ripoti ya WB kuhusu uchumi wa Afrika, ukuaji wa uchumi katika nchi zisizo katika eneo hilo unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 2.6 mwaka 2019, kutoka asilimia 2.5 mwaka 2018.

Kiwango hicho ni asilimia 0.2 chini ya kiwango kilichokuwa kimetabiriwa mwezi April 2019.

Albert Zeufack, mchumi anayesimamia masuala ya Afrika katika benki hiyo, amesema ukuaji wa uchumi kwa kiwango unaashiria mambo matatu ambayo ni pamoja na hali ya mvutano wa kibiashara unaoathiri dunia nzima, kiwango kidogo cha mabadiliko hasa usimamizi wa madeni, na athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa kama vimbunga vilivyopiga Msumbiji, Zimbabwe na Malawi mapema mwaka huu.

Ripoti hiyo inasema sababu hizo zimechangia kupungua kwa kiwango cha mauzo ya bidhaa kutoka Afrika na kiwango cha uwekezaji katika nchi za Afrika.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG