Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:15

Denmark yasitisha msaada kwa Tanzania


Rais John Pombe Magufuli
Rais John Pombe Magufuli

Denmark ambaye ni Mfadhili mkubwa wa pili kwa Tanzania imetangaza kuzuia msaada wenye thamani ya dola za Marekani milioni 10, ukieleza kusikitishwa kwake juu ya uvunjifu wa haki za binadamu na matamko ya kibaguzi yaliyotolewa na afisa wa Serikali ya Tanzania.

Uamuzi huo umekuja siku ambayo Benki ya Dunia (WB) ilisema ilikuwa imefuta mpango wa kuipa Tanzania mkopo wa Dola za Marekani milioni 300 baada ya nchi hiyo kusisitiza kuendeleza sera yake ya kupiga marufuku wasichana wajawazito kuendelea na masomo, na hivi karibuni imefanya ni kosa la jinai kuhoji takwimu rasmi za serikali.

“Nina hofia kuwa mambo hasi yanayoendelea Tanzania, la hivi karibuni ni kauli zisizo kubalika za ubaguzi kutoka kwa mkuu wa mkoa,” Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo Ulla Tornaes amesema kupitia ujumbe wake wa Twitter Jumatano.

Kwa hiyo Denmark hivi sasa itazuia Dola Milioni 9.88 ikiwa ni msaada kwa Tanzania, amesema. Denmark ilikuwa tayari imesha toa msaada wake wa nje mwaka 2017 wa kiasi cha Crown za Denmark 349.

Matamko yanayo dadisiwa yalitolewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ambaye mapema mwezi huu alitangaza operesheni dhidi ya watu wenye mahusiano ya kimapenzi wa jinsia moja katika jiji hilo, msemaji wa Waziri huyo wa Denmark ameliambia shirika la habari la Reuters.

Reuters haikuweza kuwafikia maafisa wa serikali ya Tanzania ili kupata kauli yao kuhusu kadhia hii. Hata hivyo Wizara ya Mambo ya Nje ilisema siku za nyuma kampeni ya Makonda dhidi ya watu wenye mahusiano ya kimapenzi wa jinsia moja ilikuwa ni msimamo wake binafsi na sio msimamo wa serikali ya Tanzania.

Serikali ya Rais Magufuli imekuwa ikikosolewa na wanasiasa wa upinzani na vikundi vya haki za binadamu vya kimataifa kwa kile walichosema ni kuongezeka kwa udikteta na serikali kutoweza kuvumilia upinzani. Lakini serikali inatupilia mbali madai hayo yanayo ikosoa.

XS
SM
MD
LG