Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 18:17

Rais wa Benki ya Dunia ajiuzulu


Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim
Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim

Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim amejiuzulu ghafla Jumatatu baada ya kuongoza benki inayotoa mikopo duniani kwa miaka sita.

Kim, Mmarekani, ataachia madaraka ifikapo Februari 1, miaka kadhaa kabla ya muda wake kumalizika.

Kim ni daktari mtaalam wa tiba na sayansi ya mambo ya kale ambaye siku za nyuma aliendesha miradi mbalimbali kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu na ukimwi katika nchi maskini zaidi duniani.

Alikuwa mtu wa kwanza kuongoza benki huku akiwa na uzoefu wa kupambana na umaskini kwa kuwa mstari wa mbele na pia kwa mara ya kwanza kuchaguliwa huku akiwa hajawahi kujihusisha na masuala ya siasa au fedha.

Kama mkuu wa Benki ya Dunia, aliweka shinikizo kwa taasisi hiyo kuchukua hatua zaidi katika kutokomeza hali mbaya sana ya umaskini katika nchi mbalimbali.

Katika barua yake ya kujiuzulu Kim amesema alijikita katika kutafuta njia za ubunifu kudhamini mapambano dhidi ya maradhi ambukizi na kusaidia watu walioondolewa katika makazi yao kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kadhalika amesema alifanya kazi na Umoja wa Mataifa na kampuni zinazo ongoza katika teknolojia kujiandaa kwa majanga ya njaa na kuyawezesha mataifa kuepukana na majanga hayo.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa World Bank Kristalina Georgieva atakuwa Rais wa mpito wa benki hiyo. Mwanamama huyo ni raia wa Bulgaria aliye na uzoefu wa masuala ya kifedha na maendeleo ya kimataifa.

XS
SM
MD
LG