Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 12:18

Afrika Kusini kuanda mazungumzo ya amani kati ya Russia na Ukraine


Viongozi wa nchi wanachama wa BRICS huko Brazili, tarehe 14 Novemba 2019. Picha na Sergio LIMA / AFP.

Afrika Kusini ilisema iko tayari kuandaa mazungumzo kati ya Russia na Ukraine, huku Rais wa Russia Vladimir Putin akipongeza pendekezo la amani la viongozi wa Afrika wanaotaka kumaliza mzozo kati ya nchi hizo mbili.

Khumbudzo Ntshavheni waziri katika ofisi ya Rais Cyril Ramaphosa alisema Alhamisi kwamba kiongozi huyo alizungumza kwa simu na Putin, na kwamba wako tayari kuanda mkutano wa amani.

"Lazima tukubaliane na uwezekano wa Afrika Kusini kuandaa mkutano wa amani ambao utafanyika hapa," alisema Ntshavheni.

Aliongezea kusema kwamba "Tukiwa sehemu ya mpango wa amani, na mahali utakapofanyika mkutano wa kilele huwa pamatafutwa, mahali pa kwanza unapoangalia ni uani kwako".

Kiongozi huyo wa Russia "aliukaribisha mpango wa wakuu wa nchi za Afrika na kueleza nia yake ya kupokea ujumbe wa amani".

Rais Cyril Ramaphosa alisema mwezi uliopita kwamba Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wote walikubali kuipokea timu ya amani yenye wajumbe sita kutoka barani Afrika.

Ujumbe huo uliotangazwa na Ramaphosa mwezi uliopita unajumuisha Marais wa Jamhuri ya Congo, Misri, Senegal, Afrika Kusini, Uganda na Zambia.

Ujumbe huo wa amani unajitokeza wakati Afrika Kusini inataka kuchafua sifa zake za kutoegemea upande wowote kufuatia shutuma kwamba imeelekea Kremlin.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG