Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:54

Abiria wawasili Addis Ababa kutoka Tigray, baada ya vita kusitishwa


An Airbus A350-941 aircraft of Ethiopian Airlines is pulled by a pushback tractor at Zurich Airport near Ruemlang
An Airbus A350-941 aircraft of Ethiopian Airlines is pulled by a pushback tractor at Zurich Airport near Ruemlang

Wasafiri wa kwanza wa ndege katika  uwanja wa kimataifa wa ndege wa Addis Ababa waliwasili Jumatano kutoka jimbo la Tigray baada ya ndege za shirika la ndege la Ethiopia kuanza tena safari zake.

Safari hiyo imeanza baada ya kusitishwa kwa miezi 18 tangu vita vilipoanza kwenye eneo hilo.

Tangazo hilo limetolewa siku moja baada wajumbe wa ngazi ya juu wa serikali kufanya ziara ya kwanza mkoani humo tangu kutiwa saini kwa mkataba wa amani mwezi uliopita.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la ndege la Ethiopian Airlines, Mesfin Tasew amesema kwamba safari mpya za ndege zitaziunganisha tena familia, kurejesha biashara, pamoja na kuvutia watalii, kwa manufaa ya jimbo hilo.

FILE - Mwanamke wa Kiethopia akichukua ngano baada ya kugawiwa na Jumuiya ya Misaada ya Relief Society ya Tigray. (AP Photo/Ben Curtis)
FILE - Mwanamke wa Kiethopia akichukua ngano baada ya kugawiwa na Jumuiya ya Misaada ya Relief Society ya Tigray. (AP Photo/Ben Curtis)

Tayari misaada imeanza kumiminika tena katika mkoa wa Tigray tangu kutiwa saini kwa mkataba wa amani Novemba 2, na hivyo kupunguza uhaba mkubwa wa chakula uliokuwa unashuhudiwa, pamoja na fedha , mafuta na dawa.

Hata hivyo eneo hilo lenye takriban wakazi milioni 6 bado halina huduma za umeme, simu, internet na benki kwenye maeneo mengi.

XS
SM
MD
LG