Kura za hesabiwa Madagascar kufuatia uchaguzi wa rais ulosusiwa na upinzani
Kura zinahesabiwa nchini Madagascar baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais ulosusiwa na idadi kubwa ya wapinzani. Uchaguzi umefanyika baada ya wiki kadhaa za ghasia na maandamano, na katika mji mkuu wa Antananarivo wafuatiliaji wanasema uchaguzi umefanyika kwa amani.

1
Mawakala wa vyama vya siasa katika kituo cha uchaguzi wansshangilia wakati afisa wa uchaguzi akihesabu kura mjini Antananarivo

2
Afisa wa uchaguzi wa Madagascar akihesabu idadi ya kura zilizoandikwa kwenye ubao mjini Antananarivo

3
Afisa wa uchaguzi akionyesha kura zinazohesabiwa kufuatia duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Novemba 16, 2023.

4
Mpiga kura atia saini kwenye daftari la wapiga kura alipofika kupiga kura kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Madagascar mjini Antananarivo, Novemba 16, 2023.
Forum