Maandamano na mapigano baada ya wanamgambo wa Hamas kushambulia Israel
Mapigano makali yameripotiwa kati ya jeshi la Israel na wapiganaji wa Hamas, siku ya pili baada ya wanamgambo hao kuishambulia Israel. Maandamano ya kuunga mkono pande zote mbili yamefayika katika miji mbali mbali ya dunia.

1
Maandamano ya kuunga mkono Israel yafanyika Manhattan, New York siku ya Jumapili, siku ya pili baada ya kundi la wanamgambo la Hamas kishambulia Israel.

2
Maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina yafanyika kwenye uwanja wa Times Square, huko Manhattan jijini New York siku ya Jumapili.

3
Mfululizo wa mashambulizi ya roketi yanayofanywa na wanamgambo wa kipalestina kutoka Gaza, huku makombora kutoka mfumo wa ulinzi wa Israel wa Iron Dome ukijaribu kuzuia roketi hizo kufika miji ya Israel. Oktoba 8, 2023.

4
Kifaru cha jeshi la Israel kinapiga doria karibu na mji wa Sderot baada ya wanamgambo wa Hamas kuingia kwa ghafl Israel kutoka Ukanda wa Gaza.