Shambulizi hilo lilitokea Januari 15, siku ya Jumapili. Hizi ni picha ambazo zinaonyesha namna shambulizi hilo lilivyowajeruhi na kuharibu mali ya kanisa hilo. Picha zote na mwandishi wa VOA Austere Malivika.
DRC: Shambulizi la kanisa na athari za mlipuko wa bomu kwa raia
Shambulizi la bomu katika Kanisa la Kiprotestanti mjini Kasindi, Wilaya ya Beni, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lilileta maafa makubwa kwa raia waliokuwa wanahudhuria ibada.
1
Kiatu kilichoachwa katika eneo la tukio la shambulizi la bomu kanisani DRC.
2
Kanisa la CEPAC lililoshambuliwa na wanaoshukiwa kuwa magaidi.
3
Mabaki ya viatu an viti vilivyoharibiwa na mlipuko wa bomu katika kanisa mjini Kasindi, Wilaya ya Beni, DRC.
4
Mmoja wa walioathiriwa na mlipuko wa bomu kanisani.