Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 19:29

Raia huko Ukraine katika maeneo yaliyozingirwa wameanza kuondoka


Wakaazi katika mpaka wa Ukraine na Poland
Wakaazi katika mpaka wa Ukraine na Poland

Raia katika baadhi ya maeneo ya Ukraine yaliyozingirwa na majeshi ya Russia walifanikiwa kuondoka Jumanne wakikimbia kwa kutumia mabasi au kwa miguu huku kukiwa na usitishaji mapigano wa muda.

Katika tukio moja, watu walikuwa wakiondoka katika jiji la mashariki la Sumy ambapo saa kadhaa awali shambulio la anga la Russia kwenye mtaa wa makazi ya watu liliuwa takribani raia 21, kulingana na mamlaka ya eneo hilo. Watu pia walionekana wakiondoka katika mji wa Irpin karibu na mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.

Wizara ya ulinzi ya Russia ilisema njia za ziada za uokoaji zitawekwa katika Chernihiv, Kharkiv na Mariupol. Majaribio kadhaa ya hapo awali ya kuweka njia ya watu kutoka katika maeneo ambayo yamekuwa yakikabiliwa na mashambulizi ya Russia wakati wa uvamizi wa takribani wiki mbili wa Russia nchini Ukraine yalianguka ikiwa ni pamoja na yale ya Mariupol, lengo la mashambulizi mapya ya makombora kulingana na ripoti.

Waziri wa mabo ya nje wa Ukraine, Dmitro Kuleba siku ya Jumanne aliishutumu Russia kwa kuwashikilia mateka watu 300,000 huko Mariupol jiji la takribani watu 430,000 na kuzuia uhamishaji wa kibinadamu.

XS
SM
MD
LG