Mgonjwa wa kwanza aliye hai kupandikizwa figo ya nguruwe iliyobadilishwa vinasaba amefariki miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji, hospitali ya Marekani iliyofanya kazi hiyo imesema.
Israel imeishambulia Gaza Jumamosi baada ya Marekani kuikosoa tena jinsi inavyoendesha vita huku Umoja wa Mataifa ukionya kuwa janga baya linaweza kutokea ikiwa Israel itauvamia mji wa Rafah wenye msongamano mkubwa.
Waokoaji na wapita njia walishangilia na kupiga makofi Jumamosi wakati manusura mmoja alipookolewa baada ya saa 116 kutoka chini ya vifusi vya jengo lililoporomoka nchini Afrika Kusini, ajali ambayo iliua watu 13.
Waokoaji walikuwa wakitafuta waathiriwa kwenye vifusi vya jengo la ghorofa tano katika mji wa George huko Afrika Kusini lililoporomoka siku ya Jumanne
Mashambulizi ya makombora ya Russia ya usiku kucha dhidi ya miundombinu ya nishati yamesababisha kukatika kwa umeme katika mikoa ya Ukraine ya Sumy na Kharkiv inayopakana na Russia, wizara ya nishati ya Ukraine imesema Jumatatu.
Wananchi wa Chad Jumatatu wamepiga kura katika uchaguzi wenye lengo la kumaliza miaka mitatu ya utawala wa kijeshi lakini uliosusiwa na wapinzani wa kiongozi wa kijeshi Mahamat Idriss Deby.
Wakufunzi wapya wa jeshi la Russia na vifaa vya kijeshi viliwasili nchini Niger, kulingana na televisheni ya serikali katika taifa hilo la Afrika ambalo linataka wanajeshi wa Marekani waondoke nchini humo.
Chama tawala cha Rais wa Togo Faure Gnassingbe kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa bunge, maafisa wamesema, na kumruhusu kiongozi huyo wa muda mrefu kuimarisha mamlaka yake chini ya mabadaliko ya katiba yenye utata.
Kenya Jumapili imesema kwamba idadi ya vifo kutokana na mvua kali na mafuriko ya wiki kadhaa imeongezeka hadi 228 na kuonya kuwa hakuna dalili ya afueni wakati huu.
Milipuko iliwaua watu tisa Ijumaa katika kambi ya wasiokuwa na makazi yao nje kidogo ya mji wa Goma katika eneo linalokumbwa na vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vyanzo katika eneo hilo vimesema.
Idadi ya vifo kutokana na mafuriko nchini Kenya imevuka 200 tangu mwezi Machi, wizara ya mambo ya ndani imesema Ijumaa, huku kimbunga kikielekea pwani ya Tanzania.
Wapiga kura nchini Togo leo Jumatatu wanawachagua wabunge baada ya marekebisho ya katiba yaliyoleta mgawanyiko ambapo wapinzani wamesema yanamruhusu Rais Faure Gnassingbe kuongeza muda kwa familia yake kuendeleza miongo kadhaa ya kukaa madarakani.
Jumla ya watu 118 walikuwa waathirika wa mauaji holela yaliyotekelezwa na polisi wa Kenya mwaka uliopita, makundi ya haki za binadamu ya ndani na ya kimataifa yamesema katika ripoti iliyochapishwa Jumatano, yakilaani “kutowajibishwa” kwa maafisa wa usalama waliohusika katika mauaji hayo.
Viongozi wa Ulaya wako katika siku ya pili ya mkutano hivi leo wa Baraza la EU mjini Brussels, ambapo mazungumzo hivi leo yanalenga jinsi ya kuondoa tatizo la kushuka kwa uchumi katika umoja huo na kuuzuia kuwa nyuma zaida ya China na Marekani.
Qatar inafikiria tena jukumu lake kama mpatanishi kati ya Israel na Hamas, waziri mkuu amesema jana wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Doha akiwa na mwenzake wa uturuki.
Serikali ya Burundi na Umoja wa Mataifa wameanzisha mchakato wa kuomba msaada wa ufadhili wa fedha ili kukabiliana na athari mbaya za mvua kubwa zinazonyesha kwa miezi kadhaa ambazo zimewakosesha makazi takriban watu 100,000.
Mapigano kati ya jeshi la Sudan na kikosi hasimu cha wanamgambo yaliua raia 25 katika mji wa kaskazini mwa Darfur wa El-Fasher, kundi la wanasheria wanaotetea demokrasia lilisema Jumanne.
Wataalam wa kijeshi wa Russia wamewasili Niger wakiwa wamebeba mfumo wa ulinzi wa anga pamoja na vifaa vingine kama sehemu ya taifa hilo la Afrika Magharibi kuimarisha ushirikiano wa kiusalama na Moscow, televisheni ya serikali imesema Alhamisi.
Umoja wa Ulaya umesema Ijumaa kuwa utaipatia Misri dola bilioni 1.7 kama msaada wa muda mfupi ili kuisaidia nchi hiyo kujenga uchumi wake.
Polisi nchini Ethiopia wamewakamata washukiwa 13 juu ya mauwaji ya kiongozi maarufu wa upinzani kutoka jimbo la Oromia, chombo cha habari cha ndani kimesema.
Pandisha zaidi