Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 11:18

Kenya: Idadi ya vifo kutokana na mafuriko yavuka 200


Afisa wa zimamoto akitoa maelekezo kwa wasafiri huku wakazi wakikagua barabara iliyoathirika vibaya kutokana na mvua kubwa huko Kitengela, Mei 1, 2024. Picha ya AFP
Afisa wa zimamoto akitoa maelekezo kwa wasafiri huku wakazi wakikagua barabara iliyoathirika vibaya kutokana na mvua kubwa huko Kitengela, Mei 1, 2024. Picha ya AFP

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko nchini Kenya imevuka 200 tangu mwezi Machi, wizara ya mambo ya ndani imesema Ijumaa, huku kimbunga kikielekea pwani ya Tanzania.

Mvua kubwa imenyesha Afrika Mashariki na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi ambayo yameharibu mazao, kusomba nyumba na kuwakosesha makazi maelfu ya watu.

Watu 210 walifariki nchini Kenya kutokana na “hali mbaya ya hewa,” wizara ya mambo ya ndani imesema katika taarifa, huku watu 22 wakifariki katika saa 24 zilizopita.

Zaidi ya watu 165,000 walikoseshwa makazi yao, taarifa hiyo imeongeza, huku wengine 90 hawajulikani walipo, na kuzua hofu kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi.

Kenya na nchi jirani ya Tanzania ambako watu 155 walifariki katika mafuriko, sasa zinajiandaa kukabiliana na kimbunga Hidaya, kinachosababisha mvua kubwa, upepo na mawimbi kwenye fukwe zao.

Mamlaka ya Tanzania imeonya Ijumaa kwamba Hidaya “kimejiimarisha kufikia kiwango cha kimbunga kikali,” saa tatu asubuhi kilipokuwa umbali wa kilomita 400 kutoka kusini mashariki mwa mji wa Mtwara.

Forum

XS
SM
MD
LG