Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 18:21

Uchaguzi wa wabunge wafanyika nchini Togo baada ya marekebisho ya katiba yenye utata


Mpiga kura kijana akitizama bango la kampeni lenye picha za wagombea wa uchaguzi wa bunge wa muungano wa vyama madarakani (DMP), mjini Lome, Aprili 24, 2024. Picha ya AFP
Mpiga kura kijana akitizama bango la kampeni lenye picha za wagombea wa uchaguzi wa bunge wa muungano wa vyama madarakani (DMP), mjini Lome, Aprili 24, 2024. Picha ya AFP

Wapiga kura nchini Togo leo Jumatatu wanawachagua wabunge baada ya marekebisho ya katiba yaliyoleta mgawanyiko ambapo wapinzani wamesema yanamruhusu Rais Faure Gnassingbe kuongeza muda kwa familia yake kuendeleza miongo kadhaa ya kukaa madarakani.

Uchaguzi huo umefanyika baada ya wabunge mwezi uliopita kuidhinisha mageuzi yanayounda nafasi mpya ya waziri mkuu ambayo wapinzani wanaamini imewekwa kwa ajili ya kumnufaisha rais Gnassingbe ili kuepuka ukomo wa mihula na kuendelea kukaa madarakani.

Akiwa madarakani kwa karibu miaka 20, Gnassingbe alimrithi baba yake Gnassingbe Eyadema, ambaye aliongoza kwa miongo minne kufuatia mapinduzi ya kijeshi katika taifa hilo dogo la pwani ya Afrika Magharibi.

Upigaji kura wa leo, utawachagua wabunge 113, na kwa mara ya kwanza manaibu 179 wa mikoa kutoka wilaya tano za nchi ambao pamoja na madiwani wa manispaa watachagua Baraza jipya la Seneti.

Forum

XS
SM
MD
LG