Maafa ya Ukame na Njaa
Mamilioni ya watu barani Afrika hawana uwezo wa kupata chakula cha kutosha. Somalia iko ukingoni mwa janga la njaa. Ukame nchini Kenya umesababisha serikali kutangaza hali ya hatari. Kaskazini mashariki ya Nigeria inakabiliwa na utapiamlo, na njaa imekwisha tangazwa katika baadhi ya sehemu za Sudan Kusini. Mamilioni ya watu katika bara —wengi wao wakiwa watoto—hawana chakula cha kujitosheleza. Idhaa ya Kiswahili ya VOA inawaletea ripoti hii inayoendelea kuhusu tatizo hili katika bara la Afrika katika Makala maalumu ya VOA “Njaa Barani Afrika"
Video | Afrika
19 Mei 2017