Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 10:54

Hali ya ukame Somalia inazidi kua mbaya


Mwanamke na mtoto wake wa and a boy walk past a flock of dead goats in a dry land close to Dhahar in Puntland, northeastern Somalia.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wa idraa ya huduma za dharura wanasema hali ya ukame inazidi kua mbaya Somalia, japokuwa kumekuwa na mvua katika baadhi ya maeneo nchini humo mwisho wa November.

Kumeripotiwa kuharibika kwa mazao maeneo mengi, wakati mifugo inakabiliwa na hatari ya kufa kwa ukame na pia kuna milipuko ya magonjwa.

Mwandishi wa VOA Joe De Capua ameripoti kwamba bado mazingira hayajakuwa nzuri kwa Somalia katika miaka ya hivi karibuni. Ukame umechanganyika na matukio mengi ya migogoro, iliyopelekea kwa zaidi ya watu milioni moja kuihama nchi hiyo.

Kuna kundi jingine la watu milioni moja au karibu na idadi hiyo ya wasomali ambao wamekuwa wakimbizi katika nchi za jirani na Yemen. Lakini watu wengi ambao hawajaondoka Somalia pia wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Justin Brady mkuu wa ofisi ya OCHA iliyoko Somalia, ambayo inaratibu shughuli za masuala ya kibinadamu.

Amesema kufuatia mvua zilizonyesha msimu wa Julai iliyopita, makadirio mapya yalitolewa kuonyesha idadi mpya ya wale wanaohitaji misaada ya kibinadamu.

Tathmini iliyofanywa na taasisi ya Food Security and Nutrition Analysis inaonyesha idadi hiyo kuwa ni watu milioni tano.

Hiyo ni hali nyingine ambayo haijawahi kuonekana tangu njaa iliyo ikumba Somalia mwaka 2012.

Kati ya idadi hiyo, watu milioni1.1 wanakadiriwa kukabiliwa na matatizo yanayohitaji msaada wa haraka na hiyo ni ngazi mpya ya kuvuka na yenye kutisha.

Ameendelea kusema kuwa kati ya watu milioni tano wanaohitaji msaada milioni nne wako katika hali inayojulikana kama ni ya msongo mkubwa.

XS
SM
MD
LG