Rais Biden asema hatari ya vita vya nyuklia kutokea duniani iko kiwango cha juu kabisa

Rais wa Marekani Joe Biden

Hatari ya vita vya nyuklia iko juu kabisa tangu hilo kuonekana mwanzoni mwa miaka ya 1960, Rais Joe Biden alisema Alhamisi usiku wakati Russia inaendelea kupoteza uongozi  nchini Ukraine ikiwachochea  maafisa wa Russia kujadili uwezekano wa mbinu za kutumia  silaha za nyuklia.

“Hatujawahi kukabiliwa na hali kama hii ya vita vya nyuklia tangu Kennedy na mgogoro wa Mokombora ya Cuba,” Biden alisema wakati hafla ya kuchangisha pesa mjini New York kwa ajili ya Kamati ya Kampeni ya Maseneta Wademokrat.

Rais John F. Kennedy

Mwezi Oktoba 1962 Marekani na Umoja wa Sovieti walikaribia kuingia katika vita vya nyuklia baada ya Marekani kupeleka makombora ya balistiki nchini Uturuki na Italia huku Russia ilijibu kwa kuweka makombora kama hayo nchini Cuba.

Rais Biden alisema Rais wa Russia Vladimir Putin, “mtu ambaye na mfahamu vizuri,” hafanyi mzaha anapozungumzia kutumia “silaha za nyuklia au kibaiolojia na kemikali.”

“Sidhani kama kuna kitu kama hicho wakati uwezo wa kutumia kwa urahisi silaha za nyuklia katika harakati za vita na hatuaishia katika silaha hizo,” alisema Biden.

Kombora jipya la masafa marefu kuvuka mabara ya ulimwengu RS -24 likizinduliwa kaskazini magharibi ya Russia, May 29, 2007. Kombora hili limetengenezwa kwa ajili ya kujihami dhidi ya makombora ya Marekani yaliyoko katika maeneo mbalimbali bara la Ulaya.

Akizungumza na wafadhili Wademokrat, Biden alisema yeye na maafisa wa Marekani walikuwa bado “wanajaribu kutafuta njia ya kumfanya Putin abadilishe mwelekeo” huko Ukraine.

“Ni wapi atapata njia ya kujitoa?” alisema Biden. “Wapi ataweza kufikia mahali ambapo siyo hatapata fedheha lakini pia akapoteza madaraka makubwa ndani ya Russia?”

Rais alisisitiza kuwa Marekani itaendelea kuiunga mkono Ukraine.