Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 12:05

Russia kujitengea rasmi sehemu 4 za Ukraine


Raia wa Russia wanaosajiliwa katika jeshi la nchi hiyo kwenda kupigana nchini Ukraine. Sept 26 2022. Pciha: AP
Raia wa Russia wanaosajiliwa katika jeshi la nchi hiyo kwenda kupigana nchini Ukraine. Sept 26 2022. Pciha: AP

Russia imesema kwamba maeneo manne ya Russia ambapo uchaguzi wa maamuzi ulifanyika yatajumulishwa na kuwa sehemu sehemu ya Russia kesho ijumaa.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema kwamba rais wa Russia Vladimir Putin atahudhuria sherehe rasmi ya kujumlisha maeneo hayo kuwa sehemy ya Russia.

Peskov ameambia waandishi wa habari kwamba viongozi wa maeneo hayo manne ambapo uchaguzi wa siku tano ulifanyika watasaini mikataba ya kujiunga na Russia.

Sherehe ya kusaini mikataba hiyo itafanyika katika ukumbi wa st George, Russia.

Ukraine na mataifa ya magharibi wametaja uchaguzi huo kuwa uchaguzi wa kihuni.

XS
SM
MD
LG