Ajali ya Ndege Tanzania: Watu watatu wathibitishwa kupoteza maisha

Waokoaji wamefikia eneo la ajali kuanza operesheni ya kuwatoa abiria kutoka katika ndege iliyoanza kuzama Lake Victoria. Reuters/ Stringers

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametangaza leo ingawaje hajasema watu hao waliokolewa vipi na muda gani. Vyanzo mbalimbali vya habari vemeeleza hadi sasa vifo vya watu watatu vimethibitishwa huku zoezi la uokoaji likiendelea.

Kwa upande wao mashuhuda wanasema huenda waliokolewa sekunde chache baada ya ajali kabla sehemu kubwa ya Ndege hiyo kufunikwa na maji.

Kwa upande mwingine RC Chalamila amewaomba Wananchi kuendelea kuwa watulivu maana mawasiliano na marubani walioko ndani ya ndege bado yanaendelea.

Ndege hiyo ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF ya Precision Air ambayo ilikuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Bukoba na ilikuwa katika safari ya kurudi Dar es salaam kupitia Mwanza.

Your browser doesn’t support HTML5

Juhudi za uwokozi zaendelea Tanzania kutokana na ajali ya ndege ya Precision Air

Global TV ipo eneo la tukio ambapo imeshuhudia ndege hiyo ikielea kwenye maji huku watu wakiokolewa.

Chanzo cha habari hii ni Global Publishers