Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 01:35

Ndege yenye watu 43 imeanguka katika Ziwa Victoria, Tanzania


Picha hii iliyotolewa kwenye video ya AYO TV, inaonyesha watu wakijaribu kuvuta ndege ya Precision Air iliyoanguka kwenye ziwa Victoria, Bukoba, magharibi mwa Tanzania Nov. 6, 2022.

Ndege yenye watu 43 imepoteza rada na kuanguka katika ziwa Victoria, karibu na uwanja wa ndege wa Bukoba nchini Tanzania.

Ndege hiyo ya Precision Air, ilikuwa inatoka Dar-es-salaam kuelekea Bukoba.

“Leo saa mbili karibu na dakika 20 kuelekea 25, tumepata majanga ya ndege ya Precision ATR42 ambayo ina namba za usajili 5HPWF ambayo ilikuwa inatoka Dar-es-salaam kuja ha Bukoba na ilikuwa na jumla ya watu 43. Katika hao 39 ni abiria, wawili ni wahudumu na 2 ni marubani,” amesema mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila.

Wakati tunaandaa ripoti hii, watu 26 wameokolewa na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera.

Video kenye mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakivuta ndege hiyo kwa kutumia Kamba iliyofungwa kwenye ndege huku boti zikiwa zimeizunguka. “Tunachunguza kuona kama tayiri zimeguza chini kwa udongo ili tupate utaalam mwingine wa kuivuta hiyo ndege ili iweze kutoka,” ameeleza Chalamila.

Maafisa wamesema kwamba “kuna mawasiliano kati ya marubani na wasimamizi wa safari za anga.”

Hakuna taarifa kamili kuhusu hali ya watu wengine 17 walio kwenye ndege hiyo.

Shirika la habari la serikali ya Tanzania TBC, limeripoti kwamba ndege hiyo imeanguka kutokana na hali mbaya ya hewa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG