Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 21:42

Watafiti Tanzania watathmini njia mbadala kusaidia mifugo kuhimili ukame


Mkutano wa Watafiti na watallam wa mifugo mjini Arusha, Tanzania
Mkutano wa Watafiti na watallam wa mifugo mjini Arusha, Tanzania

Watalam na watafiti wa mifugo nchini Tanzania wanalazimika kutafuta njia mbadala  ya  kuwawezesha  wafugaji  kupata  vyakula  mbala vya  kulisha mifugo  yao ambayo asili mia kubwa kwa sasa inakufa kwa njaa kutokana  na ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Watalam na watafiti wa mifugo nchini Tanzania wanalazimika kutafuta njia mbadala ya kuwawezesha wafugaji kupata vyakula mbala vya kulisha mifugo yao ambayo asili mia kubwa kwa sasa inakufa kwa njaa kutokana na ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Hatua hiyo inakuja kama moja ya utekelezaji wa maelekezo ya watendaji wa sekta ya mifugo akiwemo Dkt. Jonas Kizima ya kuwataka kutafuta suluhisho la kudhibiti janga la vifo vya mifugo linaloendelea kuwakabili wafugaji katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya kaskazini mwa Tanzania.

Bonyeza hapa chini ili kusikiliza ripoti kamili:

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:03 0:00

Mabadiliko ya tabia ya nchi yanaathiri sana uzalishaji wa mifugo hivyo lazima tafiti mbalimbali za malisho yanayofaa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na mabadiliko ya mifugo pia inayoweza kuendana na mabadiliko ya tabianchi," alisema Dkt Kizima.

Mkutano wa watafiti wa mifugo Arusha.
Mkutano wa watafiti wa mifugo Arusha.

Pamoja na hatua hiyo pia Dr Jonas akaelezea njia nyingine inayoweza kuwasaidia wafugaji kuwa ni pamoja na kuwa na bima za mifugo ili ziwasaidie kupunguza athari wakati wa majanga

"Kuna haja ya kuangalia ni namna gani bima ya mifugo inavyoweza kusaidia kukabiliana na majanga mbalimbali yanayowapata wafugaji," aliongeza.

Baadhi ya watalam wanasema kwa kushirikiana na shirika la viwanda vidogo, SIDO, wameshaanza kutumia technolojia ya kusindika chakula mbadala cha mifugo kama hatua za kukabiliana na janga hilo

Mtaalam David Lyamongi ansema; "SIDO, kwa kutumia elimu yao wameweza kutengeneza mashine ya kuweza kuchakata mazao ya ambayo yanashindwa kuhifdhiwa mfano nyanya, na pia mashine za kuchakata mabaki ya mazao ya nafaka kama mahindi maharage na mihogo na kuyatumia kulisha mifugo hasa katika kipindi kigumu kama hichi cha ukame."

Katika maeneo mengi ambayo wafugaji wanaendelea kukabiliana na uhaba wa malisho kwa mifugo yao pia wanakabliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa maji ambapo kwa sasa mabwawa yote waliyokuwa wanayategemea kupata maji yamekauka na wanalazimika kultewa maji na wasamaria wema wanaoshirikiana na serikali kwa ajili ya matumizi ya binadamu

Kwa mujibu wa viongozi na watendaji wa serikali Tanzania ni miongoni mwa nchi katika ukanda wa afrrika mashariki inayoendelea kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi hasa ukanda wa kaskazini ambapo pia inapakana nan chi ya Kenya

"Mifugo haina mipaka na na wala haijui tofauti ya nyasi za jrani na za nyumbani na ndio maana imetulazmu kufungua mipaka ili tushirikiane na wenzetu wa jiraji na afrika mashariki kwa ujumla," alisema Zabloni Nziku, Mkurugenzi wa taasisi ya mifugo.

-Imetayarishwa na Asraji Mvungi, Sauti ya Amerika, Arusha.

XS
SM
MD
LG