Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:41

Zoezi la kupiga kura Zambia liliendelea hadi usiku

Mawakala wa vyama vya siasa wanafuatilia kwa makini wakati afisa wa uchaguzi akionyesha karatasi ya kura mchakato wa kuhisabu kura ulipoanza katika kituo cha kupiga kura Lusaka, Zambia, Alhamisi Agosti 12, 2021AP Photo/Tsvangirayi Mukwazhi).

Sehemu za kupigia kura nchini Zambia ziliendelea kuwa wazi baada ya giza kungia  Alhamisi huku wapiga kura wakiwa wamesimama kwenye mistari mirefu kutekeleza zoezi la kupiga kura wakati maafisa wakianza kuhesabu matokeo.

Wapiga kura wengi walijitokeza katika mji mkuu, Lusaka, na maeneo mengine katika taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa uchaguzi mkuu huo ulio na ushindani mkali ambao rais aliyepo madarakani na mpinzani wake mkuu wamesema ni mtihani kwa uthabiti wa demokrasia ya taifa hilo.

Zaidi ya watu milioni 7, au zaidi ya asiliomia 83 ya wapiga kura wanaostahiki nchini Zambia, wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa rais na wabunge katika vituo zaidi ya 12,000, kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Zambia.

XS
SM
MD
LG