Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 12:49

Raia wa Zambia wanapiga kura katika uchaguzi wenye mvutano mkali


Kijana mmoja akifunga mlango katika eneo la Matero la makao makuu ya mgombea wa upinzani wa Zambia Hakainde Hichilema.
Kijana mmoja akifunga mlango katika eneo la Matero la makao makuu ya mgombea wa upinzani wa Zambia Hakainde Hichilema.

Wazambia wanapiga kura aljamisi katika uchaguzi wenye mvutano mkali ambapo rais na mpinzani wake mkuu wamesema ni mtihani kwa hadhi ya taifa hilo

Wazambia wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wenye mvutano mkali ambapo rais na mpinzani wake mkuu wamesema ni mtihani kwa hadhi ya taifa hilo la kusini mwa Afrika kama demokrasia thabiti.

Upigaji kura ulianza mapema leo asubuhi katika uchaguzi wa urais na wabunge katika vituo zaidi ya 12,000, pamoja na kwenye magereza. Zaidi ya watu milioni 7, au zaidi ya asilimia 83 ya wapiga kura wanaostahiki, wamejiandikisha kupiga kura, kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Zambia.

Rais Edgar Lungu anategemea kushinda kura kutokana na rekodi yake ya maendeleo ya miundombinu, hasa inayofadhiliwa na China, na usambazaji wa pembejeo za kilimo kama mbegu na mbolea kwa mamilioni ya wakulima.

Hata hivyo, nafasi yake inaweza kuwa hatarini kutokana na mabadiliko ya mabaya ya kiuchumi. Lungu, ambaye aliingia madarakani mwaka 2015, alipiga kura yake katika mji mkuu, Lusaka.

XS
SM
MD
LG