Akizungumza mbele ya kundi la wanaharakati wa haki za binadamu Jumatano wiki hii mjini Nairobi huko Kenya, Blinken alisema hata demokrasia iliyochangamka kama Kenya imekuwa hatarini zaidi kwa taarifa zisizo sahihi, ufisadi, ghasia za kisiasa, na manyanyaso kwa wapiga kura.
Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani nchini Kenya
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken anaendelea na ziara yake ya mataifa matatu akiwa tayari nchini Nigeria. Ziara yake itakayo chukua siku tano akiwa tayari amezuru Kenya, na anatarajiwa kumalizia na Senegal.
![Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akipanda ndege Uwanja wa Ndege wa Kikosi cha Anga Andrews, Maryland, Nov. 16, 2021. Akianza ziara yake itakayo mchukua siku tano akizuru Kenya, Nigeria, na Senegal.](https://gdb.voanews.com/ad3a6626-7e95-4f40-9d96-342ed37102b3_w1024_q10_s.jpg)
1
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akipanda ndege Uwanja wa Ndege wa Kikosi cha Anga Andrews, Maryland, Nov. 16, 2021. Akianza ziara yake itakayo mchukua siku tano akizuru Kenya, Nigeria, na Senegal.
![Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akihutubia katika Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi, Kenya Novemba 18, 2021. Andrew Harnik/Pool via REUTERS](https://gdb.voanews.com/f5cc2450-6d71-427f-8640-2bcc71831504_w1024_q10_s.jpg)
2
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akihutubia katika Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi, Kenya Novemba 18, 2021. Andrew Harnik/Pool via REUTERS
![Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili kufanya mkutano na Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Kiserikali kuhusu Maendeleo (IGAD) Workneh Gebeyehu (hayuko pichani) , katika Hoteli ya Sankara Nairobi, Kenya, Novemba 17, 2021. Blinken akiwa anajitayarisha kuelekea Nigeria katika ziara yake nyingine.(Photo by Andrew Harnik / POOL / AFP)](https://gdb.voanews.com/3491a28c-8843-47af-a509-f60ab8beb795_w1024_q10_s.jpg)
4
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili kufanya mkutano na Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Kiserikali kuhusu Maendeleo (IGAD) Workneh Gebeyehu (hayuko pichani) , katika Hoteli ya Sankara Nairobi, Kenya, Novemba 17, 2021. Blinken akiwa anajitayarisha kuelekea Nigeria katika ziara yake nyingine.(Photo by Andrew Harnik / POOL / AFP)
![Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akisaini kitabu cha maombolezo katika Kumbukumbu ya August 7, Nairobi, Kenya, Jumatano, Nov. 17, 2021, ikiwa ni eneo mojawapo la shambulizi la mabomu katika ubalozi wa Marekani mwaka 1998 lililoua mamia ya watu katika miji mikuu miwili ya Afrika Mashariki. Blinken alikuwa katika ziara ya siku tano nchini Kenya, Nigeria, na Senegal. (AP Photo/Andrew Harnik, Pool)](https://gdb.voanews.com/989778be-95dd-4dfc-92c7-d0b6157cf069_w1024_q10_s.jpg)
5
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akisaini kitabu cha maombolezo katika Kumbukumbu ya August 7, Nairobi, Kenya, Jumatano, Nov. 17, 2021, ikiwa ni eneo mojawapo la shambulizi la mabomu katika ubalozi wa Marekani mwaka 1998 lililoua mamia ya watu katika miji mikuu miwili ya Afrika Mashariki. Blinken alikuwa katika ziara ya siku tano nchini Kenya, Nigeria, na Senegal. (AP Photo/Andrew Harnik, Pool)