Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:58

Zelenskyy aipongeza Tume ya Ulaya kwa kukubali maombi ya Ukraine


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amepongeza mapendekezo ya Tume ya Ulaya kuipatia Ukraine hadhi ya uombaji uanachama wa Umoja wa Ulaya.

Wakati Rais wa Russia, Vladimir Putin amezikosoa nchi za Magharibi kwa kuiwekea Moscow vikwazo lakini wamepuuza uamuzi wa EU.

Washiriki wa Jukwaa la Uchumi wa Kimataifa huko St. Petersburg, Russia wakimsikiliza Rais Vladimir Putin, June 17, 2022. REUTERS/Anton Vaganov
Washiriki wa Jukwaa la Uchumi wa Kimataifa huko St. Petersburg, Russia wakimsikiliza Rais Vladimir Putin, June 17, 2022. REUTERS/Anton Vaganov

Putin alizungumza Ijumaa huko katika Kikao cha Kimataifa cha Uchumi huko St. Petersburg, ambako alizishutumu nchi za Magharibi kwa “kiburi cha kikoloni” na kujaribu kuiangamiza Russia kwa vikwazo alivyoelezea ni “upuuzi mtupu.”

Hata hivyo, alisema alikuwa “hana chochote dhidi” ya matakwa ya Ukraine kujiunga na EU.

Putin alisema “operesheni maalum ya kijeshi” nchini Ukraine itaendelea, alisisitiza uhuru wa Russia na nguvu zake pale zinapokabiliwa na kile alichokiita “uchokozi wa Magharibi.”

“Katika hali ya sasa, ukilinganisha na kuongezeka kwa hatari kwetu na vitisho, uamuzi wa Russia kutekeleza operesheni maalum ya kijeshi ilikuwa ni lazima – ugumu, bila shaka, lakini ilitulazimu na muhimu,” Putin alisema.

Alisema Marekani inajaribu kubadilisha “mwelekeo wa historia,” na ameishutumu Magharibi kwa kuchochea hisia dhidi ya Russia na “na kujihusisha kijeshi katika eneo la Ukraine.”

Alisema hayo wakati Russia ikiendelea na mashambulizi katika mkoa wa mashariki wa Donbas nchini Ukraine. Jeshi la Ukraine limesema Ijumaa mashambulizi yanaendelea katika miji muhimu ya Sloviansk na Sievierodonetsk.

Russia na washirika wake wanasema wanadhibiti takriban nusu ya Donetsk na karibu Luhansk yote, mikoa miwili ambayo inaunda Donbas. Sievierodonetsk na vijiji vinavyoizunguka ni sehemu ya mwisho ya Luhansk ambayo Ukraine bado inaishikilia.

Ukraine kujiunga na EU?

Mkuu wa Umoja wa Ulaya alisema Ijumaa kuwa Ukraine lazima ifikiriwe rasmi hadhi ya ombi lake la uanachama.

“Wote tunajua kuwa Waukraine wako tayari kufa kwa ajili ya msimamo wa Ulaya,” alisema Ursula von der Leyen, rais wa Tume ya Ulaya, wakati akiwa amevalia koti lenye rangi za kitaifa za Ukraine. “Tunataka waishi pamoja na sisi katika ndoto ya Ulaya.

Mapema Ijumaa, Zelenskyy alituma ujumbe wa tweet akipongeza uamuzi huo, na kuongeza, “ni hatua ya kwanza ya mchakato wa kujiunga na EU ambao bila shaka utaleta Ushindi karibu yetu.”



XS
SM
MD
LG