Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 22:39

Marekani imetuma msaada mwingine wa kijeshi kwa Ukraine kukabiliana na uvamizi wa Russia


Rais wa Marekani Joe Biden (R) akiwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika picha iliyochukuliwa Septemba Mosi 2021 Washington

Marekani inatuma msaada mwingine wa kijeshi wa dola bilioni moja kwa Ukraine sehemu kubwa ya msaada wa Washington ni silaha na vifaa vinavyolenga kukabiliana na hatua ya polepole lakini isiyo na huruma kwa Russia kwenye mkoa wa Donbas mashariki mwa Ukraine.

Rais wa Marekani Joe Biden alisema katika taarifa yake Jumatano kwamba alimfahamisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuhusu shehena hiyo mpya kwa njia ya simu na kwamba itajumuisha makombora ya ziada, silaha za ulinzi wa pwani, risasi na mifumo ya hali ya juu ya roketi kwa vikosi vya Kyiv ambayo inavihitaji kukabiliana na safu kubwa ya kijeshi ya Moscow.

Aidha Biden alisema Marekani inaipelekea Ukraine dola milioni 225 zaidi za misaada ya kibinadamu kuwasaidia raia wake walio katika hali ngumu ikiwa ni pamoja na maji salama ya kunywa, vifaa muhimu vya matibabu na huduma za afya, chakula, malazi na pesa taslim kwa familia ili kununua mahitaji muhimu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG