Waziri wa Fedha wa Zambaia amedai kuwa ucheleweshaji wa mchakato huo unaathiri uchumi wa nchi hiyo, gazeti la Financial Times limeripoti leo Jumatatu.
Katika mahojiano na gazeti hilo, Situmbeko Musokotwane amesema kuwa kuna haja ya kuharakaisha mchakato wa urekebishaji wa deni la nje, la takriban dola bilioni 13, akiashiria kwamba wito huo wa China ni kizingiti kwa mazungumzo ya kupunguza mikopo hiyo.
"Majadiliano kama hayo, ya ngazi za juu, yanafanya hali yetu kuwa mbaya zaidi, kwa sababu tunachotafuta ni suluhisho la haraka, na wala siyo mijadala ambayo inaweza kulivuta suala hilo," ripoti hiyo ilimnukuu Musokotwane akisema.
Lakini China ilikuwa na mtazamo tofauti. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Wang Wenbin, aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Beijing leo Jumatatu, kwamba "China daima imekuwa ikilipa umuhimu mkubwa suala la deni la Zambia.”
Facebook Forum