Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 22:36

Nchi 12 za Afrika zimeeleza mipango ya kutokomeza ukimwi kwa watoto ifikapo 2030


Nembo ikionyesha matumaini ya dawa zinazopunguza makali ya HIV
Nembo ikionyesha matumaini ya dawa zinazopunguza makali ya HIV

Azimio la Dar es Salaam lilitangazwa katika mkutano wa kwanza wa mawaziri katika Global Alliance to End AIDS in Children, unaozikutanisha nchi 12 na UNAIDS na mashirika mengine ya afya.

Nchi kumi na mbili za Afrika leo Jumatano ziliainisha mipango ya kutokomeza Ukimwi kwa watoto ifikapo mwaka 2030 kupitia programu mbalimbali za upimaji wa HIV, matibabu na kinga.

Lengo la mwaka 2030, ambalo lilitangazwa na UNAIDS mwaka jana, liliungwa mkono kwa kauli moja na wawakilishi kutoka mataifa 12 yaliyokutana jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Sisi sote katika uwezo wetu lazima tuwe na jukumu la kutokomeza UKIMWI kwa watoto," Makamu wa Rais wa Tanzania Philip Mpango aliuambia mkutano huo.

"Hatupaswi kubaki na wasiwasi. 2030 iko mlangoni kwetu," aliongeza.

Azimio la Dar es Salaam lilitangazwa katika mkutano wa kwanza wa mawaziri katika Global Alliance To End AIDS in Children, unaozikutanisha nchi 12 na UNAIDS na mashirika mengine ya afya.

Mataifa hayo 12 ni Tanzania, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Afrika kusini, Msumbiji, Zambia, Nigeria, Angola, Zimbabwe, Cameroon, na Ivory Coast.

UNAIDS ilisema katika taarifa yake kwamba kila baada ya dakika tano, mtoto mmoja anafariki kutokana na sababu zinazohusiana na UKIMWI.

XS
SM
MD
LG