Mahakama ilitupilia mbali mashtaka dhidi ya Wakroatia wanandoa wanne kufuatia maombi ya mawakili wao. Hapo awali walikana mashtaka.
Wanane hao ni pamoja na Zoran Subosic,miaka 52, mpiga gitaa katika bendi maarufu ya Hladno Pivo, au Cold Beer na Immovic Subosic,miaka 41, msimamizi, kulingana na vyombo vya habari vya Croatia. Wengine ni pamoja na Damir Magic, miaka 44, fundi umeme, Nadic Magic, 45, fundi, Ladislav Persic, 42, daktari, Aleksandra Persic, 43, mhudumu wa saluni ya nywele, Noah Kraljevic, 40, mkurugenzi wa programu na Ivona Kraljevic, 36, mtunza mbwa.
Mashitaka hayo yalidaiwa kuwa Desemba 7, mwaka jana, wanandoa hao wanne walishirikiana kuwasafirisha watoto hao. Watoto hao wadogo walikuwa wanatoka nchi jirani ya Congo na wanandoa hao walisema waliwachukua watoto hao kupitia wakili.
Facebook Forum