Mamlaka za China kutoka tume ya taifa ya afya ilifanya Mkutano na waandishi wa habari Novemba 13 kutoa ripoti ya ongezeko la matukio ya ugonjwa wa kupumua.
Mamlaka zimeelezea kuongezeka huko kunaweza kuwa kumetokana na kuondolewa masharti ya COVID -19 na mzunguko wa vimelea vinavyojulikana kama vile flu , homa ya mapafu, maambukizo ya kawaida ya bakteria ambayo kwa kawaida yanaathiri watoto wadogo , virusi vinavyoshambulia mfumo wa kupumua –RSV na vile vinavyosababisha COVID.
Wote china na WHO wamekabiliwa na maswali kuhusu uwazi wa kutoa taarifa kuhusu kesi za karibuni za COVID -19 zilizotokea katika mji wa katikati wa china – Wuhan mwishoni mwa mwaka 2019.
Forum