Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 22:34

White House yapuuzia ushiriki wa China mgogoro wa Israel na Gaza


White House inapuuzia ushiriki wa karibuni wa kidiplomasia wa China katika mzozo wa Israel, na Hamas, ikiwa sehemu ya juhudi za Beijing, kujiweka kama msuluhishi anayeaminika zaidi mashariki ya kati kuliko Marekani.

Msemaji wa baraza la usalama wa taifa la Marekani, John Kirby amesema katika mahojiano na VOA Jumatano, kwamba “tunaridhika na uhusiano wetu na wao."

Tunafurahishwa na uongozi wa Marekani katika eneo hili, na tunafurahi tuna uwezo wa kufanya kazi kupitia washirika wa kieneo ili kufikia matokeo ya manufaa kwetu sote,” mwanadiplomasia mkuu wa China, Wang Yi amekuwa akiongeza juhudi za kuleta amani Gaza, akikutana na maafisa wa kiarabu na kislamu Jumatatu, na kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano na misaada zaidi ya kibinadamu kwa Gaza kuendelea.

Mkutano wa Beijing, ni hatua ya kwanza ya ziara ya kutembelea miji mikuu ya wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG