Ripoti iliyotolewa na Human Rights Watch Novemba 22 imesema serikali ya China imekuwa kimfumo ikivunja au kufunga misikiti kote nchini China katika kampeni inayojulikana kama “Mosque Consolidation” katika miaka karibuni.
Katika baadhi ya kesi, mamlaka za kieneo zinaondoa majengo ya kiislamu, kama vile yale yenye minara inayobainisha ni ya kiislamu au kuvunja kabisa majengo kama kumbi zinazotumika kwa ibada mbali mbali.
Serikali ya China haijaondoa misikiti kama inavyodaiwa, lakini wanaifunga mingi, Maya Wang kaimu mkurugenzi wa HRW China ameiambia VOA kwa njia ya simu. Kuvunjwa au kubadilishwa kwa misikiti nchini China ni sehemu ya juhudi ya Beijing kupunguza uwepo wa Uislamu nchini humo na kuzuia ushiriki wa watu katika dini.
Licha ya wasi wasi kuhusu uwezekano wa kuufuta kabisa Uislamu nchini China, ubalozi wa China hapa Washington umesema, Beijing "inawalinda raia na uhuru wa dini kwa mujibu wa sheria."
Kwa mujibu wa nakala za nyaraka za serikali ya China, ripoti za vyombo vya habari na tafiti za kisomi, HRW imesema kuwa kampeni ina lengo la kuibadilisha misikiti kote nchini China na wazo hilo limetokea kwa Kiongozi wa China Xi Jinping katika wito wake wa mwaka 2016 akitaka serikali iwe na udhibiti dhidi ya dini.
Forum