Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 09:48

Waziri Mkuu wa Malaysia ajiuzulu


Waziri Mkuu Muhyiddin Yassin
Waziri Mkuu Muhyiddin Yassin

Waziri Mkuu wa Malaysia Muhidin Yassin amejiuzulu nafasi yake baada ya miezi kadhaa ya machafuko ya kisiasa na kupelekea kupoteza wingi aliyokuwa nao.

Lakini kujiuzulu kwake kunaweza kufungua ukurasa mpya wa kutokuwa na ukosefu wa uthabiti kwa kutokuwepo na mrithi yeyote wa wazi.

Kujiuzulu kwa Muhidin kunamaliza machafuko ya miezi 17 akiwa madarakani, ikiwa ni muda mfupi zaidi kwa kiongozi wa Malaysia lakini ilizuia juhudi za kufufua tena uchumi ulioharibika kutokana na janga, pamoja na kuzuia kuibuka tena kwa maambukizo ya COVID 19.

Mfalme wa taifa hilo la Asia kusini mashariki alimteuwa Muhidin kama Waziri Mkuu wa muda hadi pale kiongozi mwingine atakapopatikana lakini hakuweka muda maalumu.

Mfalme al-Sultan Abdullah alifuta uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi kwa sababu ya janga la COVID-19, akisema kuwa atatumia mamlaka yake ya kikatiba kuteuwa Waziri Mkuu anayeamini anaweza kuongoza wengi.

Muhidin amesema amejiuzulu pamoja na baraza lake baada ya kupoteza uugwaji mkono wa wengi katika bunge aliongeza kuwa mrithi wake hatakuwa na baraza lakini atasimamia majukumu ya kiutendaji na kumshauri mfalme hadi waziri mkuu mpya atakapoteuliwa.

XS
SM
MD
LG