Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:58

Ebola yaripotiwa Ivory Coast


Vijana wacheza mpira karibu na ufukwe wa Ivory Coast
Vijana wacheza mpira karibu na ufukwe wa Ivory Coast

Shirika la afya duniani WHO limesema Jumapili kwamba kesi ya kwanza ya Ebola imetangazwa mjini Abidjan wenye zaidi ya idadi ya watu milioni 4, ambacho ni kisa cha kwanza baada ya kipindi cha miaka 25.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, maafisa wa WHO wamesema kwamba haijabainika iwapo maambukizi hayo yana uhusiano na yale yaliyotokea mapema mwaka huu kwenye nchi jirani ya Guinea.

Mgonjwa aliyepatikana Abidjan na ambaye sasa anapokea matibabu, ni mwanamke mwenye umri wa miaka 18 anayesemekana kuwasili mjini humo Alhamisi kwa basi akitokea Guinea.

Waziri wa afya wa Ivory Coast Pierre N Gou Demba ,amesema kuwa mgonjwa huyo aligundulika kuwa na Ebola siku iliyofuata na mara moja akaanza kupokea matibabu. WHO limesema kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini iwapo maambukizi hayo mapya yana uhusiano na yale ya awali ya Guinea.

Mkuu wa WHO tawi la Afrika Dkt Matshidiso Moeti amesema kuwa ni suala la kutia wasi wasi kuona kuwa mgonjwa huyo amepatikana kwenye mji wa Abidjan.

XS
SM
MD
LG