Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 15:29

Waziri Mkuu wa Canada huenda atapoteza wingi katika bunge


Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akiongea katika kampeni ya uchaguzi huko Winnipeg, Manitoba, Canada, Sept. 19, 2021. REUTERS/Carlos Osorio
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akiongea katika kampeni ya uchaguzi huko Winnipeg, Manitoba, Canada, Sept. 19, 2021. REUTERS/Carlos Osorio

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau anaweza kubakia madarakani katika uchaguzi wa Jumatatu lakini inaonekana atapoteza wingi katika bunge.

Hii ni kufuatia kwa kampeni kali ambayo iliondoa matumaini yake ya ushindi mkubwa.

Trudeau ana utawala wa wachache, hivyo kumlazimisha kutegemea vyama vingine kufanya maelewano ya sera katika kutawala.

Huku kura za maoni mwezi uliopita zikimwonyesha akiwa mbele sana, alichochea kura miaka miwili mapema.

Waziri Mkuu alisema wapiga kura walihitaji kutoa maoni yao juu ya usimamizi wa serikali yake ya mrengo wa kushoto kati jinsi walivyoshughulikia suala la COVID-19.

Lakini hali ya kutokuwa na furaha iliongezeka juu ya kuitishwa mapema uchaguzi alishindwa kudumisha uongozi wake mkubwa.

Wataalam wa mikakati wanakubali itakuwa ngumu kushinda viti zaidi ya 338 katika Bunge.

XS
SM
MD
LG