Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 23:05

Wazimbabwe kufanya uchaguzi wa rais Kesho


Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa (kushoto) na kiongozi wa chama cha upinzani cha (CCC) Nelson Chamisa (kulia). Picha na Adrian DENNIS na Jekesai NJIKIZANA/vyanzo mbalimbali/AFP.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa (kushoto) na kiongozi wa chama cha upinzani cha (CCC) Nelson Chamisa (kulia). Picha na Adrian DENNIS na Jekesai NJIKIZANA/vyanzo mbalimbali/AFP.

Wazimbabwe wanatarajia kupiga kura katika uchaguzi mkuu Jumatano, uchaguzi ambao wengi wao wanamatumaini kuwa unaweza kumaliza tatizo la kiuchumi la muda mrefu nchini humo.

Lakini, matarajio hayo yamefifia kutokana na wasiwasi kwamba huwenda uchaguzi huo umeshapangwa ili kukipendelea chama tawala cha ZANU-PF ambacho kimekuwepo madarakani kwa zaidi ya miongo minne.

Upinzani ulipinga vikali ushindi wa Mnangagwa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2018, lakini bila ya kupata mafanikio, na wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema hali hiyo inaonekana itajirudia tena mara hii nchini humo. Chama tawala kimekanusha tuhuma za upinzani za kutokuwepo na usawa katika uchaguzi huu.

Kuna jumla ya wagombea 11 wanaowania nafasi hiyo ya kiti cha rais siku ya Jumatano, lakini vita vya kweli vipo kati ya Mnangagwa mwenye umri wa miaka 80 na Nelson Chamisa, wakili na mchungaji mwenye umri wa miaka 45 anayeongoza muungano wa upinzani wa Citizens's Coalition for Change (CCC).

Wafuasi wa kiongozi wa chama cha upinzani cha (CCC) Nelson Chamisa wakiwa katika mkutano wao wa mwisho wa kampeni Agosti 21, 2023. Picha na JOHN WESSELS / AFP.
Wafuasi wa kiongozi wa chama cha upinzani cha (CCC) Nelson Chamisa wakiwa katika mkutano wao wa mwisho wa kampeni Agosti 21, 2023. Picha na JOHN WESSELS / AFP.

Uchaguzi huo pia utajumuisha wabunge na madiwani wa halmashauri za mitaa.

Zimbabwe yenye utajiri wa madini iliwahi kuwa ni moja ya nchi zenye uchumi mzuri barani Afrika, lakini imekuwa katika msukosuko wa kiuchumi tangu mwaka 2000 wakati rais wa zamani Robert Mugabe alipoongoza unyakuzi wa mashamba yaliyokuwa yakimilikiwa na wazungu na kuwapa waafrika ambao hawakuwa na aridhi.

Mugabe aliondolewa madarakani kutokana na mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2017, baada ya kuwepo madarakani kwa muda wa miaka 37 na nafasi yake kuchukuliwa na mshirika wake wa muda mrefu Rais Emmerson Mnangagwa, lakini mabadiliko ya kiuchumi yaliyotarajiwa na wengi wakati huo hayajapatikana.

Katika uchaguzi huo utakaofanyika Jumatano, pia kumekuwa na ripoti za vitisho dhidi ya wapiga kura, hasa katika maeneo ya vijijini katika nchi hiyo yenye watu milioni 15, shirika la ufuatiliaji la Kituo cha Rasilimali za Uchaguzi (ERC) lilisema.

katika taarifa yake Jumatatu, ERC ilisema kwamba, "Kwa ujumla hisia za watu, kama ilivyobainishwa katika utafiti kadhaa pamoja na shirika la usimamizi wa uchaguzi nchini zinaonyesha kwamba watu wana imani ndogo sana katika mchakato wa uchaguzi huu."

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG