Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 20:52

Polisi Zimbabwe wachunguza shambulio dhidi ya waandishi wa habari


Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alipohudhuria kikao cha Afrika kwenye Mkutano wa Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa wa COP27, Novemba 7, 2022. AP.

Chama cha waandishi Zimbabwe kimekusanya taarifa za  waandishi kunyanyaswa au kushambuliwa na wafuasi wa chama tawala au kunyimwa fursa ya kushiriki mikutano ya kampeni

Maelezo ya waandishi wa waandishi wa habari kunyanyaswa kushambuliwa au kunyimwa haki ya kuripoti uchaguzi mkuu wa Zimbabwe yanawatia wasiwasi wachambuzi wa vyombo vya habari. Kutoka Harare Zimbabwe.

Polisi wa Zimbabwe wanachunguza shambulio dhidi ya waandishi wa habari akiwemo Annahstacia Ndlovu. Mwandishi huyu wa kujitegemea, ambaye anaripoti kwa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na Sauti ya Amerika anasema yeye na waandishi wengine walipigwa na kunyanyaswa mwezi Julai na wafuasi wa chama tawala cha Zanu-PF katika jiji la Bulawayo.

Perfect Hlongwane katibu mkuu wa Muungano wa Waandishi wa Habari wa Zimbabwe anasema shirika lake lilifanya kazi na polisi na vyama vya siasa kujaribu kuboresha uhusiano na vyombo vya habari kabla ya uchaguzi mkuu.

Lakini chama hicho kimekusanya taarifa za waandishi wa habari kunyanyaswa au kushambuliwa na wafuasi wa chama au kunyimwa fursa ya kushiriki mikutano ya kampeni.

Uchaguzi mara nyingi ni kitovu cha ukiukaji dhidi ya vyombo vya habari. Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika inasema inafuatilia hali katika mataifa kadhaa barani Afrika ambayo yamepangwa kupiga kura katika muda wa miezi 12 ijayo.

Nchini Zimbabwe taasisi hiyo inashuhudia ukiukwaji mkubwa zaidi kuliko wakati wa uchaguzi uliopita anasema Tabani Moyo.

Sheria mpya pia inasumbua watetezi wa vyombo vya habari. Mwezi uliopita Rais Emmerson Mnangagwa alitia saini kuwa sheria muswaada wa Uzalendo ambao unaharamisha kile andiko hilo linaita kuumiza uhuru na maslahi ya taifa ya nchi.

Wakosoaji wa sheria hiyo wanasema inaweza kuzuia uhuru wa kujieleza wakati wa uchaguzi na kwamba inaweza kuwa kinyume na katiba lakini wafuasi wake wanasema sheria italinda nchi dhidi ya raia wanaotaka kuwekewa vikwazo.

Forum

XS
SM
MD
LG