Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 03:58

Rais wa Iran Ebrahim Raisi kutembelea nchi tatu za Afrika


Rais wa Iran Ebrahim Raisi akiwa mjiniTehran, Iran, July 4, 2023. ( Reuters)
Rais wa Iran Ebrahim Raisi akiwa mjiniTehran, Iran, July 4, 2023. ( Reuters)

Rais wa Iran Ebrahim Raisi ataanza ziara nadra ya nchi tatu za Afrika ikiwa ni hatua mpya ya kidiplomasia ya kupunguza kutengwa kwa taifa hilo la kiislamu pamoja na kutafuta washirika wapya.

Ziara yake ya siku tatu itampeleka kenya, Uganda na Zimbabwe, na itakuwa ya kwanza ya rais wa Iran barani Afrika baada ya miaka 11. Kiongozi huyo anaandamana na ujumbe wa watu kadhaa akiwemo waziri wa mambo ya nje pamoja na wafanyabiasha mashuhuri.

Kulingana na shirika la habari la seriali la IRNA, Raisi atakutana na marais wa mataifa yote matatu wakati wa ziara hiyo. Jumatatu msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani ameelezea ziara hiyo ni ukurasa mpya ambao utaimarisha uchumi na biashara na mataifa ya kiafrika.

Ameongeza kusema kwamba ziara hiyo imechochewa na mitazamo sawa ya kisiasa kati ya Tehran na mataifa hayo matatu.

Forum

XS
SM
MD
LG