Tukio hilo ni kuonyesha hisia zao kufuatia kubakwa kwa wanafunzi watatu Ijumaa katika shule hizo.
Mwandishi wa VOA ameripoti kuwa polisi nchini Kenya wanaendelea na uchunguzi wakati bunge likishughulikia suala hili.
Kamati hiyo ya bunge iliyopewa jukumu kuangalia suala la elimu lilitumia muda mwingi Jumatano katika shule ya wasichana ya Moi ilioko Nairobi, ambako watoto wa kike watatu waliripotiwa kubakwa siku ya Ijumaa.
Kamati hiyo ilikuwa inafanya uchunguzi kujua jinsi watoto hawa walivyobakwa, na nani aliyekuwa na taarifa ambazo zingeweza kuwasaidia polisi.
Suala muhimu kwa kamati hiyo lilikuwa – ni wakati gani kitendo hicho cha ubakaji kilitokea na iwapo kuna mtu yoyote alisikia kitu chochote.