Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 10:41

Kenya yataka wakuu wa manunuzi wapishe uchunguzi


Wakenya wakiandamana kupinga ufisadi mbele ya Bunge na Mahakama ya Juu, Nairobi, Kenya, Mei 31, 2018.
Wakenya wakiandamana kupinga ufisadi mbele ya Bunge na Mahakama ya Juu, Nairobi, Kenya, Mei 31, 2018.

Serikali ya Kenya imewataka wakuu wa vitengo vya manunuzi na uhasibu katika wizara idara, wakala na mashirika yote wakae kando ili kupisha uchunguzi mpya kufanyika.

Kwa mujibu wa Standard Digital ya Kenya maafisa hao wanatakiwa pia kuchunguzwa juu ya mtindo wa maisha yao. Hili linafuatia agizo la Rais Uhuru Kenyatta aliyotoa katika maadhimisho ya Siku ya Madaraka kwamba taifa lazima lichukue hatua ya juu zaidi katika vita vyake dhidi ya ufisadi.

“Wakuu wote wa vitengo vya ununuzi na uhasibu katika wizara, idara, mawakala na mashirika ya umma wametakiwa kukaa kando mara moja. Kabla ya kuondoka katika nafasi zao, wameamrishwa kukabidhi majukumu yao kwa manaibu wao,” umeeleza waraka kutoka kwa msemaji wa serikali Mwenda Njoka.

Amri hiyo pia inamtaka wakuu wa ununuzi na uhasibu kupeleka taarifa zao binafsi katika ofisi ya Mkuu wa Utumishi wa Umma ifikapo Ijumaa wiki hii.

“Kadhalika maafisa hao wanatakiwa kupeleka taarifa zao binafsi katika ofisi ya mkuu ya utumishi wa Umma ifikapo Ijumaa, Juni 8, 2018 katika jumba la Harambee,” waraka huo umeeleza.

XS
SM
MD
LG