Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 10:27

Watu wenye silaha wateka kambi za jeshi Mali


Wanajeshi wa Mali wakiwa katika doria, wakikabiliana na waasi wa kabila laTuareg linalotaka kujitenga huko Bamako Machi 30, 2012. Picha na REUTERS/Luc Gnago.
Wanajeshi wa Mali wakiwa katika doria, wakikabiliana na waasi wa kabila laTuareg linalotaka kujitenga huko Bamako Machi 30, 2012. Picha na REUTERS/Luc Gnago.

Watu wenye silaha wameteka kambi mbili za jeshi kaskazini mwa Mali siku ya Jumapili, maafisa wawili waliochaguliwa wwameliambia shirika la habari la AFP, wakati msemaji wa muungano wa makundi lenye silaha ambayo wengi wao wanatokea kabila la Tuareg wakidai kuhusika na shambulio hilo.

Jeshi la Mali limethibitisha kupitia mitandao ya kijamii kwamba mji wa Lere, uliko katika mkoa wa Timbuktu kaskazini mwa Mali, ulishambuliwa siku ya Jumapili.

Afisa wa jeshi la Mali ameliambia shirika la habari la AFP kuwa jeshi "liko katika harakati za kukabiliana na hali hiyo."

"Baada ya mapigano, watu wenye silaha walizikamata kambi. Tunasubiri nguvu kutoka jeshini, lakini kwa wakati huu ni watu wenye silaha wanazishikilia hizo kambi," aliongeza.

Afisa utawala wa mkoa, pia alisema watu wenye silaha wamezishambulia kambi hizo mbili na kuendelea kuzishikilia.

Alisema kumekuwa na vifo lakini hakuweza kutoa idadi.

Almou Ag Mohamed, msemaji wa Coordination of Azawad Movements, muungano wa makundi yenye silaha yanayotaka kujitenga yanayoongozwa na kabila la Tuareg, amedai kuhusika na shambulio hilo.

Makundi yanayotaka kujitenga walianzisha uasi mwaka 2012, kabla ya mkataba wa amani na serikali kutiwa saini mwaka 2015. Lakini kwa ujumla, makubaliano hayo sasa yanachukuliwa kuwa ya kufa.

Mwezi huu makundi hayo yameshuhudia kuanzisha tena uhasama.

Siku ya Jumanne, makundi hayo yalianzisha mashambulizi dhidi ya maeneo ya jeshi yaliyoko katika mji wa Bourem, ambayo wanajeshi walisema waliweza kuyaondoa.

Forum

XS
SM
MD
LG