Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 06:43

Utawala wa kijeshi wakubali kurejesha demokrasia Gabon


Kiongozi wa mapinduzi ya Gabon Jenerali Brice Oligui Nguema alipoapishwa kuwa rais wa muda wa Gabon, Septemba 4, 2023. Picha na REUTERS.
Kiongozi wa mapinduzi ya Gabon Jenerali Brice Oligui Nguema alipoapishwa kuwa rais wa muda wa Gabon, Septemba 4, 2023. Picha na REUTERS.

Mpatanishi wa Afrika ya Kati kwa Gabon na kiongozi mpya wa kijeshi wa nchi hiyo wamekubaliana kuandaa mchakato wa kurejesha utawala wa kidemokrasia kufuatia mapinduzi ya wiki iliyopita, afisa wa utawala alisema.

Jenerali Brice Oligui Nguema aliapishwa Jumatatu kuwa rais wa mpito baada ya kuongoza mapinduzi ya Agosti 30 ambayo yalimaliza utawala wa nusu karne wa familia ya Bongo.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Abdou Abarry, amemwambia kiongozi wa kijeshi wa Gabon kwamba taasisi za Umoja wa Mataifa ziko tayari kuisaidia nchi hiyo katika kipindi cha mpito kurejea kwenye utawala wa kikatiba.

Mwakilishi huyo maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Afrika ya Kati, alikutana na Nguema mjini Libreville siku ya Jumatano na kumueleza kwamba Umoja wa Mataifa ungeisaidia nchi hiyo inayoanza upya.

Muungano wa mataifa yenye utajiri wa mafuta -- Mali, Guinea, Sudan, Burkina Faso na Niger ni miongoni mwa mataifa ya Afrika ambayo yamepitia mapinduzi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita – mwenendo ambao unatia wasi wasi katika bara hilo na kwingineko.

Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (ECCAS) Jumanne ilimtuma mjumbe wake, Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Archange Touadera, kwenda Libreville kwa mazungumzo na Oligui.
"ECCAS iliniteua kama mwezeshaji... kuandaa rasimu ya mchakato ya kuwezesha kurejea kwa haraka utaratibu wa kikatiba, katika makubaliano ya kuwepo kwa rais wa mpito," Touadera alisema katika hotuba fupi iliyoonyeshwa kwenye televisheni ya Gabon Jumatano jioni.

Afisa mwandamizi katika msafara wa Oligui alithibitisha kuwa, wawili hao wamekubalia kwa wakati huu kuandaa mpango huo.

Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi (wapili kushoto) ambaye ni msemaji wa serikali ya mpito, akisoma taarifa kwenye televisheni ya Gabon, Septemba 7, 2023. Picha na Gabon 24 / AFP.
Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi (wapili kushoto) ambaye ni msemaji wa serikali ya mpito, akisoma taarifa kwenye televisheni ya Gabon, Septemba 7, 2023. Picha na Gabon 24 / AFP.

Si Touadera wala afisa yeyote aliyetoa maelezo kuhusu mpango huo au ratiba ya matukio.

Mapinduzi ya Agosti 30 yaliungwa mkono na jeshi, polisi, wapinzani wa kisiasa na baadhi ya watu wa chama cha rais aliyepinduliwa Ali Bongo Ondimba, ambaye aliwekwa kizuizini na wanajeshi muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa urais uliochafuliwa kwa madai ya kuwa wa udanganyifu.

Bongo ameitawala Gabon kwa miaka 14. Alimrithi baba yake Omar, ambaye aliitawala nchi hiyo kwa miaka 41, na kupata sifa

ya kuwa kiongozi katili na aliyetumia madaraka kwa kujilimbikizia mali.

Oligui aliahidi Jumatatu kuitisha "uchaguzi huru, wa wazi na wa kuaminika" na kurejesha utawala wa kiraia lakini hakutoa muda maalum.

Jumuiya hiyo ya EECCA yenye nchi wanachama 11, ilisimamisha uanachama wa Gabon na kuamuru haraka kuhamisha makao yake makuu kutoka Gabon kwenda Equatorial Guinea, kulingana na makamu wa rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Nguema Obiang Mangue.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP na Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG