Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 22:01

Watu wasiopungua 82 wafariki katika ajali ya moto hospitali Baghdad

Mgonjwa anayeugua COVID-19 akitayarishwa kuondolewa katika gari ya wagonjwa nje ya hospitali ya Ibn Khatib, baada ya moto kuzuka kutokana na kulipuka kwa mtungi wa Oxygen Baghdad, Irak, 25 April 2021. (Foto: REUTERS/Thaier Al-Sudani)

Moto ulioanza baada ya mtungi wa oxygen kulipuka umeuwa watu wasiopungua 82 na wengine 110 kujeruhiwa katika hospitali moja mjini Baghdad iliyokuwa inavifaa vya kuwahudumia wagonjwa wa COVID-19, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani amesema Jumapili.

“Tunahitaji kwa haraka kupitia tena hatua zote za kuhakikisha usalama katika hospital zote kuepusha tukio kama hili la kusikitisha kutokea tena siku za usoni,” msemaji wa wizara Khalid al- Muhanna amekiambia kituo cha televisheni, akitoa taarifa ya vifo.

Moto huo ulizuka Jumamosi katika hospitali ya Ibn Khatib eneo la Diyala Bridge.

Watu waliojitokeza kusaidia katika ajali ya moto huko katika Hospitali ya Ibn Khatib, Baghdad, Iraq.
Watu waliojitokeza kusaidia katika ajali ya moto huko katika Hospitali ya Ibn Khatib, Baghdad, Iraq.

Ali Bayati, mjumbe wa Iraq wa Ubalozi wa Iraq unaosimamia haki za binadamu, alisema awali idadi kamili ya vifo bado haijatangazwa rasmi lakini inaweza ikawa kati ya vifo 30-45.

Ndugu za wagonjwa walikuwa wanahangaika wakati wa moto huo kuwaokoa ndugu zao wapendwa.

Mtu moja aliyekuwa anamtembelea ndugu yake alieleza jinsi watu walivyokuwa wanaruka kutoka madirishani kukimbia moto huo.

“Moto ulienea, kama vile petroli … nilimchukua kaka yangu nje mtaani, karibu na sehemu ya ukaguzi wa magari. Halafu nikarejea na kwenda tena juu baada ya hapo. Ghorofa ya mwisho, ambayo ilikuwa haijashika moto. Nikamkuta msichana hawezi kupumua, umri miaka 19, alikuwa hawezi kupumua, Alikuwa anakaribia kukata roho,” amesema Ahmed Zaki

“Nilimbeba mabegani mwangu, na kukimbia chini. Watu walikuwa wanaruka … MadaktarI waliangukia katika magari. Kila mtu alikuwa anaruka kutoka ghorofani. Na niliendelea kwenda tena juu na kuwachukua watu nakuwaleta chini tena,” Zaki amesema.

Wagonjwa walihamishiwa katika hospitali nyingine, vyanzo vya habari vilieleza. Lakini familia kadhaa zilikuwa bado hospitalini baada ya moto huo kuzimwa kwa masaa kadhaa baadae kwa kuwa hawakujua ndugu zao wako wapi.

Waziri Mkuu Mustafa al-Kadhimi ameagiza uchunguzi ufanyika juu ya moto huo.

“Tukio kama hili ni Ushahidi wa uzembe na hivyo nimeagiza uchunguzi uanze mara moja na meneja wa hospitali na viongozi wa usalama na ukarabati wa hospitali hiyo wakamatwe pamoja na wote wanaohusika mpaka pale tutakapo watambua wale waliofanya uzembe huo na kuwawajibisha,” amesema katika tamko lake.

XS
SM
MD
LG