Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Agosti 03, 2021 Local time: 18:05

Watu milioni 5 waambukizwa Corona kote duniani


Watu wakiwa katika eneo la kuogelea ikiwa ni siku moja ya kuruhusu watu kutoka nje kupunga hewa, wakati maambukizi ya COVID-19 yakiendelea huko Cologne, Ujerumani Mei 21, 2020.REUTERS/Thilo Schmuelgen

Idadi ya watu ambao wameambukizwa virusi vya Corona kote duniani imezidi milioni 5, latin Amerika ikiongoza kwa maambukizi ya kila siku kuanzia wiki iliyopita, ikifuatiwa na Marekani Pamoja na Ulaya.

Maambukizi yanaonyesha awamu mpya ya kusambaa kwa virusi hivyo, ambayo yalifikia kilele chake mwezi Februari nchini China, kabla ya kuongezeka Ulaya na Marekani.

Latin Amerika imeripoti robo tatu ya maambukizi ya watu 91,000 yaliyoripotiwa wiki iliyopita.

Ulaya na Marekani zimerekodi asilimia 20 ya maambukizi kila mmoja.

Idadi kubwa ya maambukizi imeripotiwa nchini Brazil, ambayo karibuni iliripoti maambukizi ya watu wengi kuliko Ujerumani, Ufaransa na Uingereza.

Brazil ni ya tatu duniani kuripoti idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona baada ya Marekani na Russia.

Maambukizi yanaongezeka sana nchini Brazil kila siku na kuiweka nchi hiyo katika nafasi ya pili baada ya Marekani.

Watu 326,000 wamefariki kutokana na maambukizi ya Corona kote duniani. Zaidi ya nusu ya idadi ya vifo imeripotiwa Ulaya.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Kennes Bwire, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG