Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 09:17

Idadi ya mambukizo ya corona yaongezeka duniani


Mfanyakazi wa Afya akitumia kipimo cha COVID-19 kupima maambukizi ya virusi vya corona Johannesburg, Afrika Kusini, Mei 8, 2020. (AP Photo/Themba Hadebe)

Idadi ya wagonjwa wa Covid-19 duniani imezidi million 3.9, kufikia Ijumaa na zaidi ya yatu 270,000 wamefariki huku wagonjwa million1.35 walipona, kulingana na ukurasa wa tovuti wa WorldOMeter.

Marekani bado inashika bendera kwa idadi kubwa ya yatu walioambukizwa kuliko mataifa mengine baada ya maambukizo kupindukia million 1.29 na watu 76, 942 wamefariki.

Afrika Mashariki

DRC

Katika kanda ya Afrika Mashariki na maziwa makuu, DRC bado inaongoza kwa idadi kubwa ya yatu waloambukizwa ikiwa wamefikia 897 baada ya yatu wengine 34 kuripotiwa jana. Wagonjwa 119 walipona, imesema ripoti ya kitengo cha kitaifa cha kupambana na COVID-19.

Rwanda

Katika nchi jirani ya Rwanda, wizara ya afya imethibitisha Alhamisi kwamba watu watatu wengine wameambukizwa na kufanya idadi ya walioambukizwa kufikia 271. Wagonjwa 133 walipona. Rwanda haijaripoti kifo chochote hadi sasa.

Kufuatia taarifa hizo serikali ya Rwanda inapanga kutumia maabara ya kupima virus vya HIV ili kufanya vipimo zaidi vya virus vya COVID-19. Kitengo cha kupima magonjwa ya kuambukiza, Rwanda Biomedical Center kinasema hivi sasa kinawapima kiasi cha watu 1000 kwa siku, na lengo ni kupima watu wengi zaidi.

Zanzibar

Huko Zanzibar, waziri wa Afya Rashid Mohamed ametka tarifa onayoeleza kwamba kuna wagonjwa wngie 29 waloambukizwa na hivyo kufanya idadi ya jumla kisiwani humo kufikia 134. Na idadi ya wagonjwa nchini Tanzania sasa imefikia 509.

Uganda

Uganda imeripoti mtu mimosa tu kuambukizwa Ijuma na kufikisha idadi ya wagonjwa kua 101. Wizara ya afya ya Uganda inasema mtu huyo aliyeambukizwa virusi vya corona ni dereva wa lori kutoka Tanzania.

Kenya

Kenya hadi tulipoanda ripoti hii ilikua na wagonjwa 607 wa covid 19 baada ya yatu wengine 25 kupatikana na ugonjwa huo siku ya Alhamisi.

Somalia

Somalia ndio inaonekana kukabiloiwa na changamoto zaidi kutokana na ugonjwa wa corona, kwa sabbat ya watu kutoheshimu amri ya kukaa nyumbani iliyotolewa na serekali kuu, kulingana na uchunguzi uliofanywa na gazeti la the East Africa. Kufikia Ijumaa idadi ya watu waloambukizwa nchini humo imefikia 928 baada ya kuripotiwa wagonjwa 55 mnamo siku moja hapo Ijuma.

The East African linasema watu wanaendelea kwenda miskitini kwa wingi, hasa wakati wa sala ya tarawehe wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Ulaya

Kwa épande wa Ulaya, Hispania, Italia, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi, na Sweden hazikuripoti maambukizo mapya kwa siku ya pili mfululizo Ijuma. Ubelgiji ndio inaendelea kukumbwa na maambukizi ambapo watu 591 wameambukizwa kwa siku moja na watu 106 kufariki siku hiyo.

Amerika Kusini

Huko Amerika kusini, Mexico imeripoti watu 1,982 waloambukizwa kwa siku moja na watu 257 kufaraiki siku hiyo. Imetayarishwa na

XS
SM
MD
LG