Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 16:53

Watu 6 wauawa kwa kupigwa risasi Sacramento, California


Maafisa wa usalama wajadiliana baada ya shambuzli mjini Sacramento, California

Polisi mjini Sacramento, jimbo la California, Marekani, wanasema watu sita wamekufa na wengine tisa wamejeruhiwa baada ya kupigwa risasi katikati mwa jiji hilo.

Idara ya Polisi ya Sacramento inasema ufyatuaji risasi huo, ulitokea mapema leo Jumapili.

Video iliyotumwa kwenye Twitter ilionyesha watu wakikimbia barabarani huku milio ya risasi ikisikika nyuma yao.

Video nyingine ilionyesha ambulensi nyingi zikiwa kwenye eneo la tukio. Polisi walitoa maelezo machache kuhusu mazingira ya tukio hilo, lakini walisema kupitia ujumbe wa Twitter kwamba "uwepo mkubwa wa polisi utasalia kwenye eneo la tukio, huku uchunguzi ukiendelea.”

Polisi wamesema shambulizi hilo lilitokea mwendo wa saa nane usiku wa kuamkia leo, karibu na Kituo cha Golden 1, uwanja ambapo timu ya mpira wa vikapu ya Sacramento Kings, huchezea na matamasha kufanyika.

Maafisa walisema biashara kadhaa karibu na eneo la tukio zilifungwa wakati wakifanya uchunguzi.

Tunasubiri taarifa zaidi kuhusu nini hasa kilifanyika katika tukio hili la kusikitisha," Meya Darrell Steinberg alisema kwenye Twitter.

Tukio hilo limejiri ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja baada ya mwanamume mmoja kuwapiga risasi na kuwaua watoto wake watatu na mtu wa nne kabla ya kujitoa uhai katika mji huo.

Hadi tukitayarisha ripoti hii, hakuna mshukiwa aliyekuwa ametiwa mbaroni.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG