Ni shambulizi baya la tatu katika siku za karibuni.
Siku mbili zilizopita, maafisa wawili wa polisi waliuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Hadera. Wiki moja kabla, watu wanne waliuawa kwa kuchomwa kisu katika mji wa Beersheba. Kundi la Islamic State lilidai kuhusika na mashambulizi yote mawili.
Shambulio la karibuni sana, lilifanyika katika maeneo mawili, polisi walisema, na liliendeshwa na mtu mwenye silaha aliyekuwa kwenye pikipiki.
Vyombo vya habari vya Israel viliripoti kwamba mtu huyo mwenye silaha alishambulia majengo ya ghorofa katika kitongoji cha waumini wenye itikadi kali wa Kiorthodox na baadaye akawafyatulia risasi wapita njia, shirika la habari la Reuters liliripoti.
Mshambuliaji huyo naye aliuawa kwa risasi.
Shirika la Associated Press linasema mashambulizi ya Islamic State nchini Israel ni nadra.