Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 21:06

Kenya-Waendesha boda boda 16 washukiwa wa unyanyasaji wa kingono waachiliwa huru.


Muendesha boda boda akipita kwenye barabara, wakati wa msongamano wa magari jioni jijini Nairobi, Septemba 26, 2018. Picha ya AFP.
Muendesha boda boda akipita kwenye barabara, wakati wa msongamano wa magari jioni jijini Nairobi, Septemba 26, 2018. Picha ya AFP.

Mahakama nchini Kenya Jumatatu imewaachilia huru waendesha boda boda 16 waliokamatwa kutokana na shambulio baya dhidi ya mwanadiplomasia wa kike, baada ya serikali kushindwa kutoa ushahidi wowote dhidi yao.

Waendesha boda boda walikamatwa mapema mwezi huu katika msako baada ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwaonyesha wanaume hao wakimvua nguo msichana huyo na kumpapasa, huku akipiga kelele kuomba msaada akiwa ndani ya gari lake, baada ya kulazimishwa kufungua mlango.

Mahakama ya Nairobi imeamuru waachiliwe mara moja baada ya waendesha mashtaka kusema hawakupata ushahidi wa kutosha kuhusisha waendesha boda boda hao na uhalifu.

“Kwa vile afisa aliyefanya uchunguzi hakupata ushahidi wa kushtaki washukiwa, ninawaachilia huru”, aliamuru jaji mwandamizi wa mahakama Martha Nanzushi.

Mwanaume wa 17, anayedaiwa kuwa kiongozi wa shambulizi hilo, ataendelea kukabiliwa na kesi na anakabiliwa na kifungo cha maisha jela ikiwa atakutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono.

Alikamatwa wiki mbili zilizopita karibu na mpaka wa Tanzania, kwenye umbali wa kilomita 430 kaskazini magharibi mwa Nairobi baada ya kukwepa kukamatwa kupitia mrefeji wa maji taka, polisi walisema.

XS
SM
MD
LG