Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 10:35

Maambukizi ya virusi vya corona yaongezeka duniani


Makamu wa Rais Mike Pence akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya virusi vya corona akiwa na kamati ya usimamizi ya White House katika Ikulu ya Marekani, Washington, U.S. March 2, 2020. REUTERS/Leah Millis.

Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona yamegunduliwa katika nchi zaidi wakati jjumiya ya kimataifa na serikali mbalimbali zikijaribu kuhakikisha wanadhibiti maambukizi mapya katika nchi zao.

Jumla ya majimbo 17 ya Marekani, yameripoti maambukizi ya Corona kufikia sasa, na Makamu wa Rais Mike Pence akisema jumla ya watu 150 wameambukizwa na virusi hivyo nchini Marekani hadi sasa.

Maambukizo yameongezeka nchini majimbo manne zaidi yakiripoti maambukizi mapya, huku baraza la wawakilishi likipitisa bajeti ya dola bilioni 8 kukabiliana na hali hiyo.

Imethibitishwa kwamba watu 57 zaidi wameambukizwa na virusi vya corona kote Marekani, maambukizi mapya yakiripotiwa katika majimbo ya Colorado, Maryland, Tennesee na Texas, na katika mji wa San Francisco.

Majimbo ya Texas na Maryland, yamethibitisha maambukizi ya watu sita kwa pamoja huku majimbo ya Tennessee na Colorado yakiripoti kisa kimoja katika kila jimbo.

Zaidi ya watu 98,000 wameambukizwa virusi vya Corona kote duniani, na zaidi ya 3,300 kuaga dunia, idadi kubw aya vifo – zaidi ya 3000, vikiwa vimetokea China. Kwa upande wake Itali imeripoti vifo vya watu 148.

Cameroon imekuwa nchi ya hivi punde barani Afrika kuripoti maambukizi mapya ya Corona, raia wa Ufaransa, mwenye umri wa miaka 58 aliyewasili mji mkuu wa Yaounde Februari 24, akithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Nchi zingine za Afrika ambazo zimeripoti maambukizi ya Corona ni Misri, Nigeria, Tunisia, Morocco, Senegal na Afrika kusini, na jumla ya watu 29 wameathibishwa kuambukizwa virusi hivyo, wote wakiwa wageni kutoka nje ya Afrika.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG